Rasimu, inasubiri kupitiwa na mwanasheria.

Malipo na Sera ya Kutorudisha Pesa

Imesasishwa: 26 Nov 2026

Kwa kifupi

Malipo yote kwenye DumaBoost ni ya mwisho. Haturudishi pesa taslimu wala kwenye simu. Pale tu tunaposhindwa kukupa huduma uliyolipia, kiasi hicho kinaingia kwenye salio lako la DumaBoost ukitumie kwa huduma nyingine. Sera hii haiondoi haki zako zozote chini ya sheria za Tanzania.

Kilicho bure

Kutafuta na kusoma kazi na zabuni, kubonyeza Omba, taarifa za kazi kwenye simu, kufungua akaunti na kuanza CV au barua ni bure. Usimlipe mtu yeyote ili upate kazi.

Huduma zinazolipiwa ni za mwisho

Ukishalipia na huduma ikatolewa, hairudishwi: kupakua CV au barua ya maombi, DumaBoost Pro (siku 7, siku 30, miezi 3 au mwaka 1, hata kama hujatumia siku zote), tangazo la kazi au zabuni lililokwisha onekana, kuweka tangazo juu (Maalum), vitu vilivyochapishwa, na Uhakiki wa Zabuni uliokwisha fanyika. Hii ni hivyo hata ukifunga tangazo mapema, ukipata mtu haraka au ukibadilisha nia.

Lini tunaweka kiasi kwenye salio lako

  • Tumeshindwa kuidhinisha tangazo lako kabla halijaonekana (au hatukuweza kuthibitisha kuwa tangazo lililopo ni la taasisi yako).
  • Umelipa mara mbili kwa kitu kimoja.
  • Pesa imekatwa lakini huduma haikutolewa kwa sababu ya tatizo upande wetu.

Kiasi kinaingia kwenye salio lako la DumaBoost ndani ya siku 3 za kazi, hakiishi muda, kinatumika kwa huduma yoyote ya DumaBoost na hakibadilishwi kuwa pesa taslimu. Kama ulilipa bila akaunti, fungua akaunti bure kwa namba uliyolipia ukipokee.

Hakuna salio wala marejesho

Tangazo au mwajiri aliyeondolewa kwa kujaribu kutapeli watu au kuvunja kanuni za matangazo, vitu vya bure au vya promosheni, na kazi iliyokwisha fanyika kama ulivyoagiza.

Msaada wa zabuni

Ada ya wataalamu wa zabuni inakubaliwa kwa maandishi kabla kazi kuanza, na inafuata makubaliano hayo.

Oda za zamani za mitandao ya kijamii

Kwa oda za zamani za followers, likes na views: kama hakuna kilichofika ndani ya saa 24 tunaighairi kwa mtoa huduma, na kiasi kinaingia kwenye salio lako la DumaBoost baada tu ya mtoa huduma kuthibitisha kughairi.

Umekatwa kimakosa?

Tuambie ndani ya siku 7 kupitia ukurasa wa “Wasiliana nasi”, ukiweka namba ya malipo au ya tangazo. Tunaangalia na kukujibu siku za kazi.

Taarifa za kazi

Chagua unachotaka kujulishwa. Unaweza kubadilisha au kuzima wakati wowote.

Nijulishe kuhusu

Zote zimechaguliwa. Ondoa tiki kwenye usichotaka.

Fani hizi tu (si lazima) · Mikoa hii tu (si lazima)

Acha wazi upate zote.

Bure · taarifa moja kwa saa zaidi · hakuna kati ya saa 4 usiku na saa 12:30 asubuhi