Kuhusu DumaBoost: inavyofanya kazi
Duma ni Kiswahili cha mnyama mwenye kasi kuliko wote nchi kavu. DumaBoost ni huduma ya Duma Brand, imejengwa Tanzania kwa ajili ya Watanzania.
Tunafanya mambo matatu mahali pamoja, kwa simu yako:
- Kazi na Zabuni: kutoka tovuti za ajira, kurasa za waajiri na vyanzo vya umma, zinasasishwa siku nzima, kila tangazo mara moja.
- CV na barua za maombi kwa msaada wa AI.
- Kutangaza kazi na zabuni kwa waajiri na wanunuzi, kila tangazo linakaguliwa kabla ya kuonekana. Pia msaada wa mtaalamu kushinda zabuni.
Inavyofanya kazi
DumaBoost ni nini?
Tovuti ya Tanzania inayokusanya nafasi za kazi na zabuni kutoka tovuti za ajira, kurasa za waajiri na vyanzo vya umma sehemu moja, pamoja na zana ya AI ya kuandika CV na barua za maombi, na sehemu ambayo waajiri na wanunuzi wanatangaza kazi na zabuni zilizokaguliwa.
Ni kwa ajili ya nani?
Watafuta kazi na wanafunzi wanaomaliza masomo, makampuni yanayotafuta zabuni, na waajiri au taasisi zinazotaka kutangaza kazi au zabuni Tanzania.
Natafutaje kazi?
Fungua Kazi au Zabuni, tafuta kwa neno, chagua fani, mkoa, aina ya kazi au tarehe ya mwisho. Kila tangazo linaonyesha mwajiri, mahali, tarehe ya mwisho na chanzo chake.
Naomba kazi wapi?
Kwa mwajiri moja kwa moja: kitufe cha Omba kinafungua ukurasa wa mwajiri au mnunuzi, au tunakuonyesha email yao na maelekezo ya tangazo. DumaBoost haipokei maombi yako wala haichukui ada kwa kuomba.
CV builder inafanyaje kazi?
Chagua moja ya designs 12 za CV, kisha ongea, andika au pakia CV yako ya zamani. AI inapanga na kuboresha maneno kutokana na taarifa zako tu, bila kubuni waajiri, tarehe au vyeti. Unaona CV nzima kabla ya kulipa, kisha unapakua PDF.
Barua ya maombi inafanyaje kazi?
Chagua kazi (au bandika tangazo), tumia CV yako ya DumaBoost, na AI inaandaa barua inayoendana na kazi hiyo, kwa moja ya designs 7 (ikiwemo mfumo wa barua wa Tanzania). Unaihariri kabla ya kupakua PDF au Word.
Nahitaji kujisajili?
Hapana kwa kutafuta, kusoma na kuomba kazi. Akaunti ya bure inahitajika kutengeneza CV au barua, kuhifadhi kazi, kutangaza, au kulipia huduma.
Kipi ni bure na kipi kinalipiwa?
Bure: kutafuta, kusoma na kuomba kazi na zabuni, taarifa za kazi kwenye simu, kuhifadhi kazi, na CV ya kwanza na barua ya kwanza ya kila akaunti (ofa ya uzinduzi). Kinacholipiwa: CV na barua zaidi, kutangaza kazi au zabuni, na msaada wa mtaalamu wa zabuni (ada inakubaliwa kwa maandishi). Bei inaonyeshwa kabla hujalipa.
Mnakaguaje matangazo?
Matangazo yanayowaomba watafuta kazi pesa yanazuiwa. Waajiri wanaotangaza hapa wanakaguliwa (usajili, email ya kazi, hati, simu) kabla tangazo halijaonekana. Kila tangazo lina "Ripoti tangazo hili".
Mnalindaje taarifa zangu?
CV na barua zako zinaonwa na wewe tu. Waajiri wanaweza kuona CV yako pale tu unapowasha "Ruhusu waajiri waione CV yako". Hatuuzi taarifa zako. Maelezo kamili yako kwenye Sera ya Faragha.